OTHER WEBSITE LISTS


Sunday, August 28, 2011

Mashirika ya misaada yahaha kuokoa Wasomali wanaokufa kwa njaa



· Kundi la al-Shabaab latoza misaada kodi


MAKUNDI ya watoa misaada wa kimataifa nchini Somalia yanahaha kuokoa maisha ya watoto wanaoangamia kwa njaa kali, huku wakitatizwa na kundi la kigaidi la al- Shabaab ambalo linataka wahisani wanaoingiza chakula cha misaada kulipa kodi.

Somalia imekuwa na tatizo la njaa kwa miongo sita sasa, kutokana na ukame ambao umepelekea watu zaidi ya milioni 11 kuwa katika hatari kubwa ya kupoteza maisha kutokana na ukosefu wa chakula, wengi wao wakiwa ni watoto na wazee wasiokuwa na uwezo wa kupigania chakula hicho.

Hadi sasa watu zaidi ya 1,000 wamekwisha poteza maisha nchini humo na wengine kulingana na hali kuzidi kuwa mbaya wamejikuta wakiyakimbia makazi yao na kuhamia mataifa jirani yakiwemo Tanzania na Kenya.

“Wamekuwa wakikimbia kwa kuwa wengi wamejikuta wakipoteza mifugo kutokana na ukame kuwa mkali katika maeneo mengi, na hilo limekuja baada ya kuona hakuna namna yoyote ya matumaini,” alisema Bw. Mark Bowden mratibu kutoka Umoja wa Mataifa ambaye amekuwa bega kwa bega na waathirika ili kuwapa msaada.

Alisema kwamba, kwa muda mrefu Somalia imekuwa haina mvua na si hilo tu, pia wamekuwa na migogoro ya wao kwa wao, hali hiyo imewafanya watu wengi kukumbwa na utapiamlo na ikiwa mama atakuwa na ugonjwa huo ni dhahiri kuwa hata mtoto hatokuwa na msaada.

Wasomalia wamekuwa wakilia kuomba msaada kwa watu mbalimbali, kilio chao kikubwa ni kwa UN ambapo waliiomba ijitokeze kuwasaidia ili kuokoa maisha yao na kwamba dunia iwaangalie.

Hata hivyo juhudi za UN kuiokoa Somalia zimekuwa zikikwamishwa na kundi la kigaidi la kiislamu nchini humo, al-Shabaab, kutokana na kwamba mara wanapokuwa wameleta misaada ya chakula, kundi hilo limekuwa likiwataka walipe kodi au wakati mwingine kuwaomba rushwa jambo ambalo lilielezwa kuwa, si limewakatisha tamaa watu wengi.

Watoaji wengine wa misaada nchini humo kama; shirika la mpango wa chakula ulimwenguni (UN-WFP) wamekuwa wakilalamika kwamba nchi hiyo ni hatari sana kutokana matatizo wanayokumbana nayo wakati wa kutoa misaada, huku wakilalamikia vitendo vya utekaji nyara wa mara kwa mara.

Inadaiwa kwamba watu zaidi ya kumi wamekufa kutokana na kushambuliwa wakati wa kuwasaidia wasomali wengi zaidi wamekuwa wakikimbilia Ethiopia na Kenya.

Shirika la Word Vision ni moja kati ya mengi ambayo yamekuwa yakitoa msaada kwa waathirika wa baa la njaa nchini Somalia.

Ili kuweza kutia mkono wako kwa watoto na wazee wanaokufa kwa njaa nchini Somali unaweza kutuma SMS kupiti "4africa" to 20222 pia unaweza kutembelea tovuti ya the World Vision, ama kwa kupiga simu 1-888-56-CHILD (1-888-562-4453).


Kanisa katoliki lapinga kilevi harusini


· Wasema ni wakati wa kujifunza toka TAG

JAMUIYA ya Wakarismatiki wa Kanisa Katoliki lililopo Parokia ya Mjimwema mjini hapa, wameonyesha msimamo wa kutokuweka kileo sehemu za sherehe kutokana na kwamba kufanya hivyo ni kinyume na maandiko matakatifu.

Hayo yalijidhihirisha hivi karibuni wakati wa maadhimisho ya sherehe ya agano la ndoa la mke na mume, Julita Msanga na Venansi Lihawa, katika kanisa hilo na kuhudhuriwa na waumini wengi toka sehemu mbalimbali.

Wanajumuiya hao, walisema kuwa ifike wakati wajifunze kutoka kwa makanisa kongwe ya wokovu kama Tanzania Assemblies of God, kwa kupinga kileo na kufanya mambo yao mengi kulingana na Agizo la Mungu kupitia maandiko matakatifu.

Walisema kuwa, moja ya mambo ambayo yanarudisha nyuma maendeleo ni kunywa kileo hivyo, ni lazima kama kanisa lisimame kwa nguvu zote kupinga matumizi ya kileo ili kuendana na mandiko matakatifu katika kuinua waumini kiroho tofauti na ilivyo zoeleka kwenye sherehe.

Wakiendelea kutolea mfano wa Kanisa la TAG walisema, kwa msimamo wa kanisa hilo la kupinga kileo wamefanikiwa, kwa waumini wao kuwajengea imani na maadili mema.

Aidha walisema kuwa ukweli unauma lakini nilazima wasimame kwenye njia ya kweli kwa kukemea maovu kwa vitendo na siyo hadithi au kufanya kama kazi ya mazoea siku zote za maisha.

Pia walisema kuwa kinacho uma zaidi waumini wanapo kuwa na sherehe takatifu kama hizi wanakimbilia kuandaa zawadi za nafaka maarufu kama majamanda ili wakatengenezee kileo jambo ambalo ni hatari kiimani.

Hivyo Wanakarismatiki hao waliwataka waumini kusoma maandiko matakatifu, huku akitolea mfano wa Mithali 21:23 na kuendelea zinazoeleza athari za kileo ni nini.

FBI waomba msaada wa kanisa kukamata magaidi



SIKU chache baada ya Ikulu ya Marekani (White House), kutangaza mbinu mpya ya kupambana na magaidi, Shirika la kijasusi nchini humo (FBI), limesema kwamba njia bora ya kuzuia watu hao kutoendelea na michakato yao ni kutumia dini, kutokana na kwamba wao, kwa namna moja au nyingine wanaweza kufanikiwa kwa urahisi tofauti na inavyodhaniwa.

FBI sambamba na mashirika mengine ya Kimarekani yalihimiza hilo wiki iliyopita, ambapo pia waliomba hata wadau hao watakao husika katika zoezi hilo basi wawe wanalipwa papo kwa papo.

Mapema mwezi huu Utawala wa Obama ulitangaza mpango mpya ambao waliugundua katika kuendeleza upingaji wa ugaidi nchini Marekani, ambapo Obama aliwaandikia jumuiya za waislamu walioko nchini humo ambapo watoto wao, familia zao pamoja na majirani zao kuwa ndio wanolengwa katika kuondoa kikundi cha kigaidi cha Al-Qaida na alifanya hivyo kwasababu wanalijua vizuri kundi hilo la kigaidi.

Taarifa ilitahadharisha kuwa wakati katiba ikitangaza uhuru wa kujieleza hata kwa mtu mmoja mmoja kwa habari nzuri au mbaya ni jukumu la serikali kuhakikisha inawashughulikia wale wote wanaokwenda kinyume na kufanya masuala ya kigaidi kwa kuangalia rika jinsia, na kwamba ugaidi wote unaofanywa na watu hao lazima uondoshwe.

“Njia nzuri ya kujilinda na ugaidi pamoja na imani imesha tengenezwa na inaanzia katika familia, jumuia za makundi mbalimbali na katika taasisi,” alisema na kuongeza:

“Umakini wao na uwezo wa kufanya kazi na mtu au taasisi nyingine na hata serikali, ni moja ya kipengele cha historia ya jumuiya yetu, iliyolenga uanzishaji na ushirikishaji wa mpango huu wa wazi kama kuleta changamoto kwa jamii.”

OCD adaka majambazi kwa kutumia jina la Yesu



· Amekuwa akifanya maeneo kadha wa kadha

· Wengine amekuwa akiwaongoza sala ya toba

AFISA wa Polisi, Wilaya ya Mpanda mkoani Rukwa, OCD Joseph Myovela, ameeleza kwamba njia mojawapo na nzuri ya kuweza kuwakamata majambazi kwa urahisi ni kutumia jina la Yesu; ambapo kwa utaratibu huo amefanikiwa kukamata majambazi sugu wengi na hata wengine kuwaongoza sala ya toba.

Akiongea na Jibu la Maisha wiki iliyopita wakati wa mahojiano maalum kwa njia ya simu toka Mpanda, mkuu huyo wa Polisi alisema kwamba, katika maeneo mbalimbali ambayo kwa namna moja ama nyingine amewahi kufanyia kazi alikuwa akitumia njia hiyo ambayo ni nyepesi.

“Unajua siku zote naangalia maandiko matakatifu yanasema nini, katika Zaburi 127:1 Neno linaeleza kwamba: “Bwana asipoulinda mji yeye aulindaye akesha bure,” nikimshirikisha Bwana kwa kweli huwa nawakamata kwa urahisi kabisa,”

Mkuu huyo wa Polisi alibainisha kwamba, njia hiyo ambayo amekuwa akiitumia kwa muda mrefu, ilisaidia kumponya Polisi mmoja Jonas Mathias aliyekuwa akitumika Ngara mkoani Kagera aliyegubikwa na nguvu za giza lakini kwa jina la Bwana Yesu alifanikiwa.

Akielezea mkasa uliompata Polisi huyo, ambaye baada ya wakuu wake huko Ngara kuona hali yake inakuwa mbaya zaidi, walilazimika kumpa ruhusa ili arudi kupata matibabu kijijini kwao kata ya Mamba, alisema kwamba mwishoni mwa mwezi wa Saba Askali huyo alikwenda kituoni kwao ilikuomba msaada.

“Askari Mathias alikuja ofisini kwetu akiletwa na mkewe ambaye alituambia kwa ufupi matatizo ambayo mume wake alikutana nayo na kwamba wanahitaji msaada,” alisema na kuongezea:

“Nilimwambia kumbe taarifa niliyopewa na mkuu wa kituo cha Ngara mtu mwenyewe ni yeye, nilimwambia m ke wake kwamba tatizo alilonalo mumewe ni mapepo ambayo kwa jina la Yesu pekee ndio tiba kinyume na hapo basi ataendelea kuteseka.”

Alieleza kwamba alimchukua askari huyo na kwenda nae nyumbani kwake na kushinda nae huko akimuombea , ambapo mkewe alirudi nyumbani kuangalia familia.

“Nilipoanza kumwombea ghafla alianguka na kupoteza fahamu, lakini mimi niendelea kumwombea kwa muda mrefu; alikuwa ni kama hajitambui kabisa sikujali hilo niliendelea kukemea, na wakati zoezi hilo likipamba moto ghafla alianza kupiga kelele sana,” alisema na kuongeza:

“Kwa kweli ilikuwa kazi sana, lakini namshukuru Mungu, mwisho wa siku aliamka na kuuliza kwamba alikuwa wapi jambo ambalo hakuwahi kulifanyika tangu alipokumbwa na mapepo na kulazwa kwa takriban miezi miwili mkoani Kagera.”

Alisema baada ya Bwana Yesu kumponya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kiasi cha kumaliza waganga lakini kuendelea kuteseka alieleza kuwa, alipopata ufahamu kuwa alikuwa wapi aliomba simi na kumpigia mkewe ili kumpa taarifa ya hali yake.

Sambamba na hilo alitanabaisha kwamba, mke wake baada ya kusikia kwamba mume wake anaongea, alifurahi sana na kuamua tangu siku hiyo kuokoka na kumgeukia Bwana Yesu.

OCD ambaye ni muumini wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Mpanda alisema baada ya Bwana Yesu kumfungua Askari huyo, alitoa taarifa kwa OCD wa Ngara na kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, ambao walishindwa kuamini kwamba kwa maombi tu ameweza kupona.

Akisimulia mkasa mzima uliompata hadi kufikia hatua ya kurudishwa kijijini wao, Polisi huyo, Jonas Mathias alisema, siku moja akiwa mkoani Kagera wilayani Ngara, alikuwa katika matembezi yake ya kawaida, usiku wa saa moja na musu ghafla alikutana na watu watatu lakini hakuwajali na kwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwake, alipofika mlangoni aliwaona kwa mara nyingine wamesimama mlangoni.

“Nilishtuka kidogo lakini sikuwajali na kuamua kuingia ndani, nililala na baada wiki moja nikiwa tena kwenye matembezi yangu nilikutana na mtu mmoja akiwa amembeba abilia na nilipowakaribia

Yule aliyebekwa alianza kubadilika na kuwa katika sura za wanyama kama Simba, Fisi nap aka,” alisema nakuongeza:

“Mimi nilipoona wananighasi nilimshika paka na kumkaba sawasawa, sikumwachia nilimshika kwa nguvu hadi nyumbani, na nilipoingia ndani nilimwambia mke wangu anipe kisu na nilipoanza kumchinja; kisu kikakunjika, sikuishia hapo nilifanikiwa kumchinja na kumweka mezani.”

Aliongeza kwamba baada ya kumchinja na kwenda kulala, majira ya saa tisa usiku ghafla katika dirisha lake alihisi watu wakizunguka zunguka, ambapo hakujua wametoka wapi na aliona aende nje ili kujua kulikoni.

Sambamba na hilo alisema kwamba, alipofika nje hakuona watu na aliorudi kuangalia mezani alikokuwa amemuweka yule paka hakuwapo na aliachana nae na kwenda kuendelea kulala.

Hata hivyo baada ya tukio hilo, siku sita baadaye akiwa nadani amekaa ghafla allizingirwa na wimbi fulani na ghafla alijikuta yuko baharini, akiwa huko ni kama alikuwa na ufahamu nusu kwani alichokuwa akitambua kwa mbali ni kuwa haya ni maji.

Wale walioonekakana kama ni watu walimtesa huko kwa kutaka kubadilisha miguu na mikono yake lakini ilikuwa ikikataa kufanyika vile walivyokuwa wakitaka wao; walikuwa wakimkaba na kupiga.

Sambamba na hilo baada ya kuona hafi kama walivyokuwa wakitaka, walimpeleka eneo lingine ambalo hakulijua na wakamuingiza kwenye gesti na huko alimfanyia mateso ya kutosha ikiwa ni pamoja na kunyweshwa dawa na pombe lakini kwa neema ya Mungu alipoteza fahamu.

“Wahudumu wa ile hoteli baada ya kuona ni muda mrefu kwamba sitoki katika kile chumba ambacho sikuwa nikijua kwamba niliingia saa ngapi waliamua kugonga bila mafanikio na ndipo walipoamua kuita Polisi na kuvunja mlango,” alisema na kuongeza:

“Walipoingia na kuniamsha nilipata fahamu kwa mbali sana na wakaniuliza mimi ni nani kweli sikuweza kuwajibu isipokuwa niliwaonyesha kwa vitendo kuwa, nilikuwa ni Polisi wa Kagera, walipiga simu huko na kuwaambia kuwa, nilikuwa Shinganya, na ni siku sita tangu nilipo potea.

Alisema kwamba alikuja kuchukuliwa na kupelekwa katika hospitali akiwa hana uwezo wa kuongea wala kusikia kabisa, alikaa hospitali kwa muda wa miezi miwili lakini hali yake haikuwa na dalili zozote za kupona; mwisho wa siku wakuu wake wa kazi waliamua kumrudisha kwao Mpanda ili kuendelea na matibabu zaidi.

“Namshukuru Mungu kunileta huku kwetu, nilikuwa ni kama nusu mfu, OCD ameniokoa na sasa nimeamua mumpa Yesu maisha yangu.” Alimalizia

Friday, August 12, 2011

waumini hawa wa kanisa la Bethel Baptist wakiomba huku wakiwa wameinamisha vichwa vyao chini katika mji wa Spanaway kwenye beach ya Cranberry,kusini mwa bahari ya Pasifiki wakati mtoto Dale Ostrander, mwenye miaka 12 alipozama kwa dakika 20 na alipop[elekwa hospitali huku ndugu zake wakiomba aliweza kuwa mzima kiasi cha kuwashangaza madaktari.