OTHER WEBSITE LISTS


Monday, October 31, 2011

Kijana Gadson anahitaji msaada wako


Mtajwa hapo juu ambaye kwa majina ni Gadson Gamson kisodya kutoka mkoani Kigoma, anahitaji msaada wako wa hali na mali, ikiwa pesa au maombi ili aweze kwenda India kutibiwa kutokana na maumivu makali aliyonayo baada ya kuanguka kutoka juu ya mwembe alipokuwa katika michezo ya watoto shuleni, miaka nane iliyopita.


  1. Ajali hiyo ilimsababishia maumivu makali ya uti wa mgongo na hatimaye ulemavu kuanzia kiunoni hadi miguuni, kiasi kwamba kutokwa haja kubwa na ndogo bila kujijua, sambamba na vidonda vikubwa, kama vinavyoonekana pichani.

Alitibiwa hospitali ya Mkoa wa kigoma, Maweni bila mafanikio kisha alilazwa hospitali ya taifa muhimbili kitengo cha mifupa MOI kwa miaka miwili (2) matokeo hayakuleta tumaini. Madaktari wa Muhimbili wamemuandikia rufaa ya kufanyiwa upasuaji nchini India. Ambapo itahitajika kiasi cha jumla ya Tsh. Mil. 13.

Kama utaguswa na kutaka kumsaidia basi mchango wako utufikie kabla ya 16 November 2011 kupitia

Obadia kabuga 0768 119 908/0764 466610

No comments:

Post a Comment