OTHER WEBSITE LISTS


Sunday, August 28, 2011

Kanisa katoliki lapinga kilevi harusini


· Wasema ni wakati wa kujifunza toka TAG

JAMUIYA ya Wakarismatiki wa Kanisa Katoliki lililopo Parokia ya Mjimwema mjini hapa, wameonyesha msimamo wa kutokuweka kileo sehemu za sherehe kutokana na kwamba kufanya hivyo ni kinyume na maandiko matakatifu.

Hayo yalijidhihirisha hivi karibuni wakati wa maadhimisho ya sherehe ya agano la ndoa la mke na mume, Julita Msanga na Venansi Lihawa, katika kanisa hilo na kuhudhuriwa na waumini wengi toka sehemu mbalimbali.

Wanajumuiya hao, walisema kuwa ifike wakati wajifunze kutoka kwa makanisa kongwe ya wokovu kama Tanzania Assemblies of God, kwa kupinga kileo na kufanya mambo yao mengi kulingana na Agizo la Mungu kupitia maandiko matakatifu.

Walisema kuwa, moja ya mambo ambayo yanarudisha nyuma maendeleo ni kunywa kileo hivyo, ni lazima kama kanisa lisimame kwa nguvu zote kupinga matumizi ya kileo ili kuendana na mandiko matakatifu katika kuinua waumini kiroho tofauti na ilivyo zoeleka kwenye sherehe.

Wakiendelea kutolea mfano wa Kanisa la TAG walisema, kwa msimamo wa kanisa hilo la kupinga kileo wamefanikiwa, kwa waumini wao kuwajengea imani na maadili mema.

Aidha walisema kuwa ukweli unauma lakini nilazima wasimame kwenye njia ya kweli kwa kukemea maovu kwa vitendo na siyo hadithi au kufanya kama kazi ya mazoea siku zote za maisha.

Pia walisema kuwa kinacho uma zaidi waumini wanapo kuwa na sherehe takatifu kama hizi wanakimbilia kuandaa zawadi za nafaka maarufu kama majamanda ili wakatengenezee kileo jambo ambalo ni hatari kiimani.

Hivyo Wanakarismatiki hao waliwataka waumini kusoma maandiko matakatifu, huku akitolea mfano wa Mithali 21:23 na kuendelea zinazoeleza athari za kileo ni nini.

No comments:

Post a Comment