OTHER WEBSITE LISTS


Sunday, August 28, 2011

OCD adaka majambazi kwa kutumia jina la Yesu



· Amekuwa akifanya maeneo kadha wa kadha

· Wengine amekuwa akiwaongoza sala ya toba

AFISA wa Polisi, Wilaya ya Mpanda mkoani Rukwa, OCD Joseph Myovela, ameeleza kwamba njia mojawapo na nzuri ya kuweza kuwakamata majambazi kwa urahisi ni kutumia jina la Yesu; ambapo kwa utaratibu huo amefanikiwa kukamata majambazi sugu wengi na hata wengine kuwaongoza sala ya toba.

Akiongea na Jibu la Maisha wiki iliyopita wakati wa mahojiano maalum kwa njia ya simu toka Mpanda, mkuu huyo wa Polisi alisema kwamba, katika maeneo mbalimbali ambayo kwa namna moja ama nyingine amewahi kufanyia kazi alikuwa akitumia njia hiyo ambayo ni nyepesi.

“Unajua siku zote naangalia maandiko matakatifu yanasema nini, katika Zaburi 127:1 Neno linaeleza kwamba: “Bwana asipoulinda mji yeye aulindaye akesha bure,” nikimshirikisha Bwana kwa kweli huwa nawakamata kwa urahisi kabisa,”

Mkuu huyo wa Polisi alibainisha kwamba, njia hiyo ambayo amekuwa akiitumia kwa muda mrefu, ilisaidia kumponya Polisi mmoja Jonas Mathias aliyekuwa akitumika Ngara mkoani Kagera aliyegubikwa na nguvu za giza lakini kwa jina la Bwana Yesu alifanikiwa.

Akielezea mkasa uliompata Polisi huyo, ambaye baada ya wakuu wake huko Ngara kuona hali yake inakuwa mbaya zaidi, walilazimika kumpa ruhusa ili arudi kupata matibabu kijijini kwao kata ya Mamba, alisema kwamba mwishoni mwa mwezi wa Saba Askali huyo alikwenda kituoni kwao ilikuomba msaada.

“Askari Mathias alikuja ofisini kwetu akiletwa na mkewe ambaye alituambia kwa ufupi matatizo ambayo mume wake alikutana nayo na kwamba wanahitaji msaada,” alisema na kuongezea:

“Nilimwambia kumbe taarifa niliyopewa na mkuu wa kituo cha Ngara mtu mwenyewe ni yeye, nilimwambia m ke wake kwamba tatizo alilonalo mumewe ni mapepo ambayo kwa jina la Yesu pekee ndio tiba kinyume na hapo basi ataendelea kuteseka.”

Alieleza kwamba alimchukua askari huyo na kwenda nae nyumbani kwake na kushinda nae huko akimuombea , ambapo mkewe alirudi nyumbani kuangalia familia.

“Nilipoanza kumwombea ghafla alianguka na kupoteza fahamu, lakini mimi niendelea kumwombea kwa muda mrefu; alikuwa ni kama hajitambui kabisa sikujali hilo niliendelea kukemea, na wakati zoezi hilo likipamba moto ghafla alianza kupiga kelele sana,” alisema na kuongeza:

“Kwa kweli ilikuwa kazi sana, lakini namshukuru Mungu, mwisho wa siku aliamka na kuuliza kwamba alikuwa wapi jambo ambalo hakuwahi kulifanyika tangu alipokumbwa na mapepo na kulazwa kwa takriban miezi miwili mkoani Kagera.”

Alisema baada ya Bwana Yesu kumponya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kiasi cha kumaliza waganga lakini kuendelea kuteseka alieleza kuwa, alipopata ufahamu kuwa alikuwa wapi aliomba simi na kumpigia mkewe ili kumpa taarifa ya hali yake.

Sambamba na hilo alitanabaisha kwamba, mke wake baada ya kusikia kwamba mume wake anaongea, alifurahi sana na kuamua tangu siku hiyo kuokoka na kumgeukia Bwana Yesu.

OCD ambaye ni muumini wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Mpanda alisema baada ya Bwana Yesu kumfungua Askari huyo, alitoa taarifa kwa OCD wa Ngara na kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, ambao walishindwa kuamini kwamba kwa maombi tu ameweza kupona.

Akisimulia mkasa mzima uliompata hadi kufikia hatua ya kurudishwa kijijini wao, Polisi huyo, Jonas Mathias alisema, siku moja akiwa mkoani Kagera wilayani Ngara, alikuwa katika matembezi yake ya kawaida, usiku wa saa moja na musu ghafla alikutana na watu watatu lakini hakuwajali na kwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwake, alipofika mlangoni aliwaona kwa mara nyingine wamesimama mlangoni.

“Nilishtuka kidogo lakini sikuwajali na kuamua kuingia ndani, nililala na baada wiki moja nikiwa tena kwenye matembezi yangu nilikutana na mtu mmoja akiwa amembeba abilia na nilipowakaribia

Yule aliyebekwa alianza kubadilika na kuwa katika sura za wanyama kama Simba, Fisi nap aka,” alisema nakuongeza:

“Mimi nilipoona wananighasi nilimshika paka na kumkaba sawasawa, sikumwachia nilimshika kwa nguvu hadi nyumbani, na nilipoingia ndani nilimwambia mke wangu anipe kisu na nilipoanza kumchinja; kisu kikakunjika, sikuishia hapo nilifanikiwa kumchinja na kumweka mezani.”

Aliongeza kwamba baada ya kumchinja na kwenda kulala, majira ya saa tisa usiku ghafla katika dirisha lake alihisi watu wakizunguka zunguka, ambapo hakujua wametoka wapi na aliona aende nje ili kujua kulikoni.

Sambamba na hilo alisema kwamba, alipofika nje hakuona watu na aliorudi kuangalia mezani alikokuwa amemuweka yule paka hakuwapo na aliachana nae na kwenda kuendelea kulala.

Hata hivyo baada ya tukio hilo, siku sita baadaye akiwa nadani amekaa ghafla allizingirwa na wimbi fulani na ghafla alijikuta yuko baharini, akiwa huko ni kama alikuwa na ufahamu nusu kwani alichokuwa akitambua kwa mbali ni kuwa haya ni maji.

Wale walioonekakana kama ni watu walimtesa huko kwa kutaka kubadilisha miguu na mikono yake lakini ilikuwa ikikataa kufanyika vile walivyokuwa wakitaka wao; walikuwa wakimkaba na kupiga.

Sambamba na hilo baada ya kuona hafi kama walivyokuwa wakitaka, walimpeleka eneo lingine ambalo hakulijua na wakamuingiza kwenye gesti na huko alimfanyia mateso ya kutosha ikiwa ni pamoja na kunyweshwa dawa na pombe lakini kwa neema ya Mungu alipoteza fahamu.

“Wahudumu wa ile hoteli baada ya kuona ni muda mrefu kwamba sitoki katika kile chumba ambacho sikuwa nikijua kwamba niliingia saa ngapi waliamua kugonga bila mafanikio na ndipo walipoamua kuita Polisi na kuvunja mlango,” alisema na kuongeza:

“Walipoingia na kuniamsha nilipata fahamu kwa mbali sana na wakaniuliza mimi ni nani kweli sikuweza kuwajibu isipokuwa niliwaonyesha kwa vitendo kuwa, nilikuwa ni Polisi wa Kagera, walipiga simu huko na kuwaambia kuwa, nilikuwa Shinganya, na ni siku sita tangu nilipo potea.

Alisema kwamba alikuja kuchukuliwa na kupelekwa katika hospitali akiwa hana uwezo wa kuongea wala kusikia kabisa, alikaa hospitali kwa muda wa miezi miwili lakini hali yake haikuwa na dalili zozote za kupona; mwisho wa siku wakuu wake wa kazi waliamua kumrudisha kwao Mpanda ili kuendelea na matibabu zaidi.

“Namshukuru Mungu kunileta huku kwetu, nilikuwa ni kama nusu mfu, OCD ameniokoa na sasa nimeamua mumpa Yesu maisha yangu.” Alimalizia

No comments:

Post a Comment