OTHER WEBSITE LISTS


Monday, July 11, 2011

ASKOFU ASEMA HATMA YA TZ IKO MIKONONI MWA KANISA

MAKAMU Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God, Dk. Magnus Mhiche, ameonya kuwa Taifa la Tanzania haliwezi kufikia malengo ya kiuchumi, wala kuwa na maisha bora ikiwa halitabadilika kimaadili na kumgeukia Mungu aliyeliumba, na kanisa ndilo lenye jukumu la kuwafundisha watu kuacha njia mbaya na

kumgeukia Muumba wao.

Askofu DK. Mhiche, aliyasema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Idara ya Uanafunzi na Maandiko, ya kanisa la TAG, uliofanyika Highland Camp, Morogoro wiki iliyopita na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka kila kona ya Tanzania.

Dk. Mhiche alionya kuwa, kanisa lisipochukua nafasi yake kuwafundisha na kuwajenga Watanzania katika maadili ya Neno la Mungu, ambalo lina nguvu za kuwabadili kimaadili juhudi zote za kuinua uchumi na kukabiliana na ugumu wa maisha zitakuwa bure.

Huku akinukuu maadiko matakatifu, Asna kumgeukia Muumba wao.

Askofu DK. Mhiche, aliyasema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Idara ya Uanafunzi na Maandiko, ya kanisa la TAG, uliofanyika Highland Camp, Morogoro wiki iliyopita na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka kila kona ya Tanzania.

Dk. Mhiche alionya kuwa, kanisa lisipochukua nafasi yake kuwafundisha na kuwajenga Watanzania katika maadili ya Neno la Mungu, ambalo lina nguvu za kuwabadili kimaadili juhudi zote za kuinua uchumi na kukabiliana na ugumu wa maisha zitakuwa bure.

Huku akinukuu maadiko matakatifu, Askofu Muhiche alisema kuwa, kanisa nalo lina changamoto ya kurejea katika maadili yake ili liweze kusimama katika nafasi yake ya kuliwezesha taifa kurejea katika maadili mema na idara hiyo ya Uanafunzi na maandiko ndiyo yenye dhamana ya kuhakikisha kuwa kanisa linarejea katika maadili na misingi ya upentekoste halisi.

Alisoma Neno la Mungu kutokaa katika kitabu cha Yeremia 9:23-24. Andiko hilo linasema: “…Mwenye hekima asijisifu katika hekima yake au mwenye nguvu asijisifu katika nguvu zake au tajiri asijisifu katika utajiri wake. Lakini yeye ajisifuye ajisifu na ajisifu kwa sababu hii: Kwamba ananifahamu na kunijua mimi, kwamba mimi ndimi Bwana, nitatenda wema, hukumu na haki duniani, kwakuwa napendezwa na haya asema Bwana.”

Askofu Dk. Mhiche alisema kuwa, kama mtu akiwa na mambo yote bila kumjua Mungu ni bure na ni hasara kubwa.

“Idara ya Maandiko na Uanafunzi ndicho chombo cha kutuwezesha kumjua Mungu; kwa maana kitalisaidia Taifa na kuliwezesha kanisa kuondokana na sherehe za msisimko wa kidunia, zisizo na mguso wa Roho Mtakatifu,” alisema Askofu huku akisisitiza kuwa ni wajibu wa idara hiyo kuleta uamsho kanisani ili watu wamjue Mungu na wenye wito maalumu wa kitumishi waingie kazini, wakiwa wameandaliwa vizuri.

Askofu alitaja faida kadhaa zinazotokana na kumjua Mungu ambazo ni: “Kuwa na amani, mema kukujia, Mungu kuwa hazina yako, Bwana kuwa fedha ya thamani kwako, utajifurahisha katika mwenyezi, uso wako utainuliwa kwa Mungu, utasikilizwa maombi yako, mwanga utaziangazia njia zako, nawe utakusudia neno nalo litathibitika.”

Kisha aliongeza: “Wakati huu tulio nao sio wa kuzalisha huduma zenye imani potofu, kwakuwa tunayo idara iliyopewa wajibu wa kutoa mafundisho sahihi, kufundisha watu kuabudu, misingi ya imani na itikadi safi.”

Askofu huyo aliongeza kuwa baadhi ya huduma ambazo zinaupotofu wa imani zimeanzishwa na watu waliotoka TAG, hivyo imetosha kanisa ni lazima lisimame katika nafasi yake likifundisha kweli ya Mungu ambayo itawafanya kuwa na hofu ya Mungu.

Dk. Mhiche alitoa changamoto mbalimbali kwa kanisa, kupongeza na kuhimiza Idara ya Uanafunzi na Maandiko kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa inafanya kazi katika kila kanisa la mahali pamoja ili kuhakikisha kuwa kusudi la kuanzishwa kwake linatimia.

“Idara hii ya Maandiko na Uanafunzi ni nyeti sana, ni moyo wa kanisa, ukiondoa Idara ya elimu ambao mtakaofanikisha Mpango Mkakati wa TAG; kwa maana ya kulea wanaokolewa kwa mafundisho sahihi, pia kutengeneza njia kwa watu ya kuweza kumtumikia Mungu,” alisema Dk. Mhiche na kuongeza kuwa wakati huu siyo wa kuzalisha viongozi wa Imani potofu, bali ni wakati wa kuandaa watumishi wazuri kimafundisho na itikadi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maandiko na Uanafunzi, Mchungaji Elingarame Samuel Munisi, akifunisha Somo la Uamsho kwa wakurugenzi na maofisa wengine wa idara hiyo kutoka kila kona ya Tanzania alisema kuwa; kama TAG haitaimarisha Ibada zenye nguvu za Roho Mtakatifu, itakuwa kama dini za kawaida na wala haitaweza kutofautishwa na wengine wasio wapentekoste, hivyo kuhimiza uamsho kwa kila mtu binafsi kuchukua hatua za makusudi za kumtafuta Mungu.

Akifundisha kwa mifano Mchungaji Munisi alisema: “Unapoona timu ya mpira imefanikiwa kutwaa vikombe vingi na kuwa bingwa mwenye kuheshimika sana, ukiichunguza utagundua jambo moja kubwa sana, ambalo ni juhudi za kila Mchunguji mmoja mmoja na hivyo ndivyo ilivyo hata kwenye uamsho. ni lazima kila mtu kufanya juhudi binafsi za kuudhi mwili kuuambia hapana mimi ni mwana uamshi ni lazima niutafute uamsho kwa gharama.”

Kisha aliongeza: “Uamsho sio taratibu za kidini, na wala sio mifungo mirefu, mikesha mingi na kuimba sana; hayo mengine ni matokeo ya uamsho, uamsho halisi ni kuzingatia na kumrudia Mungu ndani ya moyo. Kumpenda Mungu kunahitaji upendo wa kweli kama wa wanandoa ambao hautaki shirika, unadai kujali na wakati wote unapopungua pengo huonekana.”

Kabla ya kufundisha, Mkurugenzi huyo alisoma taarifa za utendaji mbele ya wajumbe na kisha wakajadili mambo kadha ambayo yalipitishwa na kikao cha Halimashauri kuu ya Idara iliyokutana siku moja kabla ya mkutano huo.

Lakini moto wa aina yake ulilipuka wakati Katibu mkuu wa Idara hiyo, Mchungaji Mgembe, aliposimama jukwaani kuhubiri kwa mfumo wa kiinjilisti somo la Uamsho kwa staili ya kiinjilisti iliyoambatana na maonyo ambapo utukufu wa Mungu ulifunika eneo hilo na wajumbe wote wakazama katika uwepo wa Roho Mtakatifu kwa namna ya kipekee.

Huku akisisitiza viwango vya utakatifu na uaminifu kwa imani na maadili ya upentekoste wa kweli, Mchungaji Magembe ambaye amekuwa akizunguka katika mataifa mbali mbali ya Afrika katika program kubwa ya uamsho wa kipekee barani Afrika uliobatizwa jina la “Afrika kumepambazuka” alisema kuwa; kanisa la Tanzania linapaswa kuwa makini na kuchukua hatua za makusudi kurejea katika maadili kwa kuwa Upentekoste wa kwanza unahatari ya kupotea.

“Ukiona jamii inahitaji uamsho ujue kuna tatizo, zamani wakati wa kanisa la kwanza hatukuwa na fundisho la uamsho. Ni lazima kanisa la sasa lirejee katika misingi ya upentekoste halisi wa kwanza,” alisema Mchungaji Magembe na kusisitiza kuwa bila ya Roho Mtakatifu hakuna Upentekoste.

Mkutano huo iliongozwa na andiko kutoka katika Biblia kitabu cha Warumi 13:11-14; lisemalo: “… usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi natuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.”

Miongoni mwa walioongoza mkutano huo ni Makamu Mkurugenzi, wa Idara ya Uanafunzi na Maandiko Dk. Joseph Kimeme, Askofu wa TAG Jimbo la Morogoro, Braison Msuya, Wakurugenzi wa Idara hiyo kutoka majimbo mbali mbali ya kanisa la TAG, wakurugenzi wa sehemu na wale wa kanisa la mahali pamoja.

Wajumbe mbali mbali waliohudhuria mkutano huo wa pili tangu idara hiyo kuanzishwa na Mchungaji Munisi kuteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa kwanza walieleza kufurahishwa na mafundisho na jumbe zilizotolewa katika mkutano huo ambazo ziliwakumbusha wajibu wa kipekee waliopewa na Mungu katika utumishi wao.

No comments:

Post a Comment