OTHER WEBSITE LISTS


Tuesday, July 26, 2011

sitasahau nilivyowatoa watoto wangu kafara (3)

WIKI iliyopita tulikuletea sehemu ya tatu ya ushuhuda wa Bw. Renatus Mungai, aliyesomeshwa katika hekalu la Freemasons la Nairobi, akalitumikia kwa miaka kadhaa, lakini pia akatoa kafara watoto wake watatu na sasa anajuta akiwa amekimbilia Tanzania. Anasema kuwa visa vyake na kundi hili ndivyo vilivyochangia Rais wa zamani wa Kenya Dainel Moi, kuunda tume maalumu ya kuchunguza waabudu shetani, ambayo ilihoji hadi maofisa kadhaa kutoka Tanzania. Leo katika sehemu ya 3, anaeleza jinsi alivyomficha mkewe siri kubwa kuhusu vifo vya wanae, aliowatoa kafara kama ishara ya mapenzi yake kwa shetani.


kweli huo ndio uliokuwa mtihani wangu wa kwanza, nikifikiria nitamchukuaje mtoto bila mama yake kujua? Baba aliniambia nimwambie mke wangu kuwa, tupokezane kumpeleka mtoto klini, ili na mimi nizoee zoezi hilo bila hata yeye kujua, ili nitakapoenda kliniki niunganishe safari.
Nilipofikiria niliona hiyo ndiyo iliyokuwa njia sahihi,lakini nikajiuliza atakubali? Na hata akikubli! si atataka mwezi wa kwanza aende yeye au twende wote? Nilipozingatia hilo nilibaini kuwa, hata njia hiyo nayo haitafanikiwa.
Nilimshirikisha rafiki yangu mmoja ambaye niliamini kuwa yeye ni “Mastermind” ambaye pia ni mtu wa hekalu aliyekuwa ametolewa huko na wazazi wake akiwa mdogo na alikuwa na akili sana.
Rafiki yangu huyo wa zamani ambaye kwa sasa ni miongoni mwa wanasiasa wanaotingisha siasa za Kenya, tena akipewa nafasi kubwa ya kugombea urais kwenye uchaguzi ujao, alitengua kitendawili hiki kwa sekunde tu, yeye alikuwa amekwisha tengeneza mpango makini uliofanikisha kila kitu………
Aliniambia: “usihangaike mimi nitakuchorea mpango ambao ukiufuata utafanikiwa. Mpango wenyewe ni huu, siku ya Kliniki ni kesho na ni siku hiyo uliyoamriwa kumpeleka mtoto hekaluni na Master, sasa wewe mtie moyo mkeo kuwa ajitahidi kuamka mapema ili muwahi Kliniki mapema.
Nitakupa kidonge cha usingizi ambacho kina nguvu sana, mkikaribia kuondoka nyumbani hakikisha unamuwekea kwenye soda au juisi anywe halafu akishapanda kwenye gari atashikwa na usingizi mzito utaenda naye hadi hekaluni utamuacha kwenye gari na utamchukua mtoto hadi ndani utafanya unalotaka kisha utapita Kliniki na kurudi bila yeye kujua kwa kuwa ile dawa itaisha nguvu baada ya saa 10 tangu mtu anywe na inapoisha pia itahitajika masaa mawili hivi mpaka kurudiwa na akili kamili.”
Nilipozingatia nilibaini kuwa ulikuwa ni mpango makini ambao ungeniwezesha kuendelea kuitunza siri yangu mbele ya mke wangu familia na hata wakwe zangu ambao walikuwa ni watu waliookoka wanaosali katika kanisa la Kipentekosti.
Nilimshukuru na akaniambia nifuatane naye hadi hekaluni mahali ambapo vifaa muhimu vya kazi vilikuwa vikihifadhiwa.Ingawa mimi nilikuwa mashuhuri sana hekaluni ni mahali nilipokulia baada ya kukabidhiwa huko na babu yangu nikiwa na miaka kumi sikujua kumbe kuna kitengo cha kushughulika na biashara kubwa za dawa ikiwa ni pamoja na zile za kulevya.
Tulipofika Hekaluni aliniambia nisubiri nje ambapo alifungua mlango akaingia ndani ambapo alikwenda moja kwa moja kwenye madhabahu na kusogeza meza maalumu iliyokuwa mbele ya madhabahu ile na kisha kutoa mfuko wa plastiki uliokuwa na madawa kadhaa akanikabidhi.
Niliamua kumhoji dawa ile ilitengenezwa wapi kwa kuwa haikuwa na karatasi ya maelezo na wala kasha lenyewe kuonesha athari zake wala tarehe ya kuharibika kwake. Alipoona ninamashaka aliniambia nisubiri kidogo, akaingia ndani na kutoka na kabrasha la kuhifadhia vyeti.
Alilishika na kunionesha akisema: “mimi ni Daktari niliyebobea kwenye masuala ya utafiti, uchanganyaji dawa ninaweza hata kukoroga dawa hizi mwenyewe bora tu umpe baada ya chai na apumzike kidogo.”
Nilichukua dawa ile na kuhifadhi ndani ya pochi langu mahali ambapo nilijua kuwa hakika mke wangu asingeliweza kuiona, kibarua kikubwa kilikuwa ni jinsi ya kumnywesha asubuhi asubuhi.
Nilipofikiria sana nilikumbuka kuwa anapenda sana soda za makopo na kwa kuwa anafuga kucha ndefu asingeweza kufungua kopo, nilifunga safari kwenda hadi kwenye supermaketi nikanunua katoni nzima ya soda na nikaenda nazo nyumbani.
Nilipofika alipokea kwa shangwe akanikumbatia na kuniambia: “Asante mume wangu kwa zawadi nzuri, lakini utakuwa ukinifungulia si unakumbuka zilivyokata kucha zangu.”
Nilicheka nikamwambia usijali mimi ndio jibu la matatizo yako yote nitakufungulia, leo moja na ya pili kesho wakati tunaenda Kliniki wakati mimi nikiendesha gari wewe utakuwa unakunywa koka baridi kwa raha zako.
Moyoni nilijiambia; kajisafishia njia kuelekea katika usingizi ili nitekeleze matakwa ya master maana kugombana naye kunamaanisha mwisho wa maisha huru.
Asubuhi yake tulikunywa chai safi tukajiandaa kwa ajili ya safari ya kwenda kliniki nilimshauri mama aandae maziwa na chupa kwa ajili ya mtoto, lakini aliniambia kuwa maziwa hayakuwepo kwa kuwa kopo la mwisho liliisha jana yake. Bila kusita nimsihi tupitie dukani tukanunue, ila yeye achukue maji ya moto kwenye chupa kwa ajili ya kuchanganyia. Nilijua kuwa masaa nane au kumi ambayo atakuwa amelala mtoto atahitaji chakula na sisi akina baba hatuna maziwa, ni lazima nitengue kitendawili hicho pia.
Niliendesha gari hadi kwenye supermarket nikanunua maziwa nikaangalia na chupa ya kuweka nikamwambia mke wangu anielekeze jinsi ya kuchanganya ili siku nyingine ni msaidie. Alipomaliza kunielekeza na wakati huo akiwa ameshamnyonyesha mtoto kashiba yuko kwenye kiti chake maalumu nyuma nikachukua kopo la soda huku kidonge nikikibana na kidole cha kati nikalifungua na kuvuta funda mbili kisha kwa ujanja sana nikatumbukiza kidonge na kutingisha.

Itaendelea

Kwa maelezo zaidi piga simu: 0753 747 524.





No comments:

Post a Comment