OTHER WEBSITE LISTS


Sunday, July 3, 2011

Ujumbe hatari wasambazwa nchi nzima

WAKATI Waziri Mkuu, Mizengo Kayanda Pinda, akipongezwa kwa kuweka wazi mchakato wa kufikia katiba mpya ya Tanzania itakayozinduliwa April 26, mwaka 2014, Mkanda wa video uliorekodiwa katika mfumo wa DVD, wenye ujumbe wa ‘hatari’ unaotia sumu mchakato huo umesambazwa kwa kasi kubwa jijini Dar es Salaam, na miji ya jirani, Jibu la Maisha limebaini.

Katiksa mkanda huo unaoonyesha picha za wahusika kwa ufasaha wakizungumza kwa kupongezana pia wanamshambulia maaskofu nchini, Kanisa Katoliki, Aliyekuwa mgombea wa urais katika uchaguzi uliopita Dk. Willbroad Slaa, CHADEMA, na Rais wa awamu ya Kwanza, Hayati Mwl. Julius Kambarege Nyerere.

Waandaaji wa mkanda huu wanadaiwa kuwa ni Jumuia za kadhaa za kiislamu zilizoitisha makongamano katika mikoa mbali mbali siku chache baada ya maandamano yaliyofanywa na CHADEMKA arusha na kupinga uchaguzi wa Meya wa mji huo na kusababisha mauaji. Na hoja inayotawala katika makongamano hayo ni pamoja na maandamano hayo ambayo wanadai yana mkono wa baadhi ya maaskofu.

Masheikh na wanazuoni mashuhuri wa jijini Dar es Salaam, (majina tunayahifadhi kwa sasa) wameonekana wakizungumza kwa ukali, huku wakionya kuwa hawataridhia katiba mpya ikiwa haitatamka wazi wazi kuhusu kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi inayotambulika kisheria na Tanzania kuruhusiwa kujiunga na OIC.

Wanadai kuwa watahakikisha kuwa watasimama kidete kuizuia katiba ili kuhakikisha kuwa wanapata haki yao ya kuwepo kwa mahakama za Kadhi na safari hii hawawezi kusikia busara wala ahadi yoyote ile kwa kuwa uvumilivu wao umefikia mwisho.

Baadhi ya mambo yaliyopo kwenye mkanda huo hatuwezi kuyaandika kutokana maadili yanayotuongoza katika tasnia hii ya upashanaji wa habari.

Wakizungumzia hayati, Mwl. Nyerere, walidai kuwa aliwahi kushauri Nigeria igawanywe kuwa mataifa mawili, la Waislamu na la Wakristo, mara baada ya kuibuka kwa vita ya Biafra.

Pia wanamuelezea kiongozi huyo wa kwanza wa Tanzania kuwa alisimika mfumo wa Kikristo ambao ulikuwa ukikandamiza watu wengine wasio Wakristo hasa katika eneo la elimu na Afya.

Wakiongea kwa kupokezana viongozi hao walitaka serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), na serikali yake kukumbuka mauaji ya Mwembe chai na Unguja wanaposhughulikia suala la mauaji ya Arusha.

“Tumekutana hapa jumuiya zote za Waislamu, wawakilishi kutoka mikoa yote…..tutajadili mambo yetu na kutumia tukio la Arusha kama “Case Study”. siku chache zilizopita kulitokea maandamano ya kisiasa Arusha na watu watatu walikufa. Watu wa Arusha wanajua lililotokea…..Maaskofu walikuja juu wakatoa kauli nzito na viongozi wa serikali wakaja juu wakasema maaskofu waombwe radhi wamevunjiwa heshima sana.….”alisema mmoja wa Masheikh waliohudhuria.

Wakinukuu hotuba wanayodai kutolewa na uongozi wa Kanisa Katoliki mbele ya kiongozi wa kanisa hilo Ulimwenguni Hayati Papa Yohane Paulo II, alipotembelea nchini walidai kuwa moja ya mambo yaliyotajwa ni kamati ya majeshi ya ulinzi ya Kanisa Katoliki.

“Sisi kama Waislamu wa jamii ya nchi hii tunatakiwa tujiulize tunajambo gani la kufanya ili kuhakikisha kuwa tunaishi kwa usalama baina ya sasa na mustakabali……hali ya sasa ya usalama si nzuri kuna kila dalili kuwa amani na utulivu vimo ukingoni,”alisema mmoja wa viongozi hao.

Walidai kuwa Suala la OIC, limezimwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam, Polycap Kadinali Pengo, ambaye alimuita Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Akielezea DVD hiyo, Mwinjilisti kutoka taasisi ya Biblia ni Jibu, Bw. Eleotori Kobelo, alisema kuwa yeye ameziona DVD hizo zilizorekodiwa katika makongamano hayo ambazo ni zaidi ya 20 zikiwa na maudhui yanayofanana yakielekeza mashambulizi kwa viongozi wengine wa dini hasa maaskofu.

“Mimi nautazama mpango huu kama jambo la hatari sana kwa kuwa unahamasisha watu kutengana kwa sababu ya imani zao. Ni jambo la hatari sana kushawishi watu kuwaona viongozi wengine kuwa ni maadui…makongamano mengine kama lile la Morogoro lilikuwa na sura tofauti. Lilihudhuriwa na mwandishi wa Televisheni ya Kimataifa ya Al-jazeera na mwingine wa Moroko, sijui ni kwanini jambo hili limechukua sura ya kimataifa,”alihoji Mwinjilisti huyo.

Juhudi za kumpata Polcapy Kadinali Pengo kujibu hoja kadhaa zilizoelekezwa kwake hazikufanikiwa mara moja na juhudi zinaendelea.

No comments:

Post a Comment