OTHER WEBSITE LISTS


Friday, July 1, 2011

Sitasahau nilivyotoa watoto wangu kwa shetani Nairobi

KARIBU kwenye ukurasa huu ambao tunakuletea mambo ya kustaajabisha yaliyowapata wale waliokuwa wakimtumikia shetani. Tunayaandika haya ili kuwasaidia wana wa Mungu ambao ndio windo kubwa la waabudu shetani hasa katika nyakati hizi za mwisho ambapo shetani huabudiwa dhahiri na ‘biblia’ yake inauzwa bila kificho. Fuatilia ushuhuda huu wa Bw. Renatus Mungai ambaye anajuta kwa kutoa watoto wake watatu kafara kwenye hekalu la waabudu shetani huko Nairobi Kenya. Endelea…

KATIKA mahojiano marefu na Bw. Renatus Mungai, alisema kuwa ni mtanzania kwa kuzaliwa ingawa wazazi wake ni wazaliwa Kenya katika eneo la Kisii na sehemu kubwa ya maisha yake aliishi nchini humo.

Huku akibubujikwa na machozi ya huzuni, Mungai alisema: “Nilizaliwa eneo la Same mkoani Kilimanjaro, Januari mwaka 1960, hapo ni mahali ambapo wazazi wangu walikuwa wakiishi na kufanya kazi na biashara zao.

Mama yangu alikuwa muuguzi katika Hospitali ya Wilaya Same, wakati baba alikuwa mfanyabiashara wa mbao akisafirisha kwenda Dar es Salaam, na maeneo mengine. Mimi ni mtoto pekee kwa wazazi wangu, na nilikuwa nikiishi kwa raha mustarehe hadi mwaka 1970, wazazi wangu wote wawili walipotangulia mbele ya haki katika ajali mbaya ya gari iliyotokea Namanga mkoani Arusha.

Baada ya kufariki kwa wazazi wangu nilichukuliwa na Babu na Bibi, kwenda Kenya kuishi nao huko. Nikiwa Kenya nilikuwa muumini wa kanisa la Anglikana pamoja na familia, lakini pia nilikuwa nikienda kwenye Hekalu kuabudu pamoja na Babu nilipofikia darasa la 10.

Niliendelea vyema na nilipomaliza sekondari nilienda Uingereza kusoma Diploma ya Juu ya Takwimu, babu aliniambia kuwa amepata ufadhili kwenye hekalu, hivyo nitakapokuwa London nitapokelewa na kulelewa na hekalu la kule mpaka nitakapomaliza.

Ingawa nilikuwa mwanachama wa kawaida, lakini nilipokaribia kwenda Uingereza nilitakiwa kutimiza masharti kadhaa ili niweze kupanda ngazi kwa kuwa ufadhili unategemea pia nafasi ya ngazi uliyonayo ambayo inatokana na uaminifu kwenye dini.

Nilihangaika kutimiza masharti ikiwa ni pamoja na kualika wanafunzi wenzangu ili kuingiza idadi kadhaa ya wanachama ambalo ni mmoja ya sharti la kupanda daraja. Nashukuru kuwa nilifanikiwa kutimiza masharti yote na hatimaye nilienda London Uingereza kusoma kwa ufadhili wa hekalu.

Nilipokuwa naondoka nchini, kuelekea London niliambiwa kuwa nikifika tu uwanja wa ndege nitapokelewa na wenzangu wanaosoma nchini humo kwa ufadhili wa hekalu….niliondoka Nairobi kwa shingo upande kuelekea London kutokana na ukweli kuwa sikuwa na dola za Marekani 400 tu, ambazo zilikuwa hitaji la lazima ninapoingia nchini humo.

Hata hivyo nilishangaa nilipotua tu uwanja wa ndege wa London, niliulizwa na karani mmoja ikiwa mimi ndiye Mungai, nikawaambia ndiye akaniambia ndugu zako wale pale….huku akinyoosha kidole kuonesha kundi la vijana waliovalia nguo nyeusi nadhifu. Walinifuata na kunikumbatia wakiniambia kuwa wao ndio jamaa zangu waliopewa jukumu na hekelu la London kunihakikishia maisha bora niwapo masomoni hapo.

Masomo yangu yalikuwa ya miaka mitatu katika chuo Kikuu cha Oxford na ingawa malipo yake yalikuwa makubwa sana na maisha ya London yalikuwa ya ghali sana, niliishi kwa raha na amani na sikuwahi kuulizwa ada wala jambo lolote kwa kuwa hekalu lililipia kila kitu.

Baada ya kumaliza masomo yangu nilirejea nchini Kenya na kuajiriwa katika moja ya idara nyeti, lakini kukiwa na makubaliano rasmi kati ya mwajiri na hekalu kuwa nitakuwa hapo kwa maslahi ya hekalu na nilikuwa naweza kufanya kazi za hekalu hata kwa mwaka mzima.

Nilioa kwa sherehe kubwa sana iliyosimamiwa na babu ambaye niliporejea kutoka masomoni nilikuta maisha yake yamebadilika sana na kuwa miongoni mwa watu wenye kipato kikubwa zaidi na alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri mjini Mombasa, ambapo alihamishiwa kuwa msimamizi mkuu wa hekalu.

Itaendelea……

No comments:

Post a Comment