OTHER WEBSITE LISTS


Sunday, July 3, 2011

Mzungu aangua kilio akihofia mbu Dar

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mzungu mmoja kutoka nchini Finland, amejikuta akishindwa kuzuia hisia zake kiasi cha kuangua kilio, baada ya kuona sehemu aliyoandaliwa kuishi kwa takriban wiki mbili atakazokuwa Tanzania, iko uswahilini, huku ikizingirwa na mbu wenye njaa kali ambao wangeweza kumdhuru yeye pamoja na mwanae mwenye umri mdogo.

Tukio hilo la aina yake lilitokea Ijumaa iliyopita Kijitonyama maeneo ya Sayansi jijini Dar es Salaam, wakati mzungu huyo (jina tunalihifadhi) alipofikishwa eneo hilo majira ya saa tatu usiku, mara baada ya kuwasili nchini Tanzania akitokea Finland na mumewe ambaye ni mtanzania sambamba na mtoto wao mdogo.

Mwandishi wa Jibu la Maisha ambaye alikuwa miongoni mwa watu waliokwenda uwanja wa ndege wa Mwl. Nyerere kumpokea mzungu huyo pamoja na mumewe mwenyeji wa Iringa, lilishuhudia mzungu huyo huku akiwa amemkumbatia mwanae akitoa machozi huku akimsihi mwanae huyo, aliyekuwa amembeba asijali kwani ingawa alikuwa akili lakini watakuwa salama tu.

“Ooh!... my baby….. don’t worry ……we will be ok!…. Inspite of these mosquito” hayo ni baadhi tu ya maneno yaliyokuwa yakisemwa na mzungu huyo huku akilia akimtaka mwanae asijali kulia kwake ili naye asilie, ingawa mbu wanaonekana ni wengi ,”

Wakati kilio hicho kikiendelea mawifi wa mzungu huyo walikuwa na kibarua kikubwa cha kumtia moyo (kumnyamazisha) mzungu huyo asiendelee kulia huku wakimwambia kwamba kesho yake wangemtafutia nyumba nyingine sehemu nzuri anayotaka ili aweze kuishi kwa amani

“Jamani ….. yaani huku Sayansi ni uswahilini! ……chumba hiki mbona kina hadhi, sisi mbona tunaona ni eneo zuri, lakini unajua kilichotuangusha ni hawa watu waliopewa pesa ili wamtafutie ‘Apartment’ inaonekana walifanya ndivyo siyo,” alisema wifi mkubwa wa mzungu huyo mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo jitihada za kumbembeleza mzungu huyo zilizaa matunda, baada ya mume wake kumwambia kwamba walale pale Kijitonnyama usiku ule na kwamba kesho yake wangekwenda kutafuta sehemu nyingine ambayo wataishi kwa amani kwa kipindi kifupi cha wiki mbili watakachokuwa nchini Tanzania.

Huku akionyesha kubali kwa kusitasita mzungu huyo aliingia ndani ya chumba hicho, ambacho kwa namna ya kawaida hakikuwa kibaya kama jinsi alivyokuwa akikichukulia, na kuanza kupekua kila mahala kama kuna mbu wamejificha, huku akiangalia kwa makini maeneo ya madirishani, bafuni sambamba na kitandani.

Hadi Mwandishi wa Jibu la Maisha anaondoka eneo la tukio, mzungu huyo alikubali kulala maeneo hayo ya Kijitonyama kwa mapatano ya siku hiyo moja tu, na kwamba kesho yake waliondoka na kwenda kukaa Masaki, eneo ambalo alilifurahia na kudai kuwa halina mbu ambao wangeweza kumletea madhara makubwa.

No comments:

Post a Comment