OTHER WEBSITE LISTS


Thursday, July 28, 2011

TANGAZO MAALUM

Uongozi wa kanisa la TAG, unapenda kuwatangazia ziongozi, Wachungaji na Washirika wake kote Tanzania na Umma kwa ujumla kuwa, kitabu kipya kilichoandikwa na Rev. Jotham Mwakimage , kiitwacho THE HISTORICITY OF TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD CHURCH, kinapotoa historia ya kweli ya kanisa letu, na kinalengo la kuvuruga juhudi za utekekezaji wa dira ya maendeleo ya kanisa letu, na mshikamano mzuri uliopo baina ya wachungaji na viongozi wao.

jopo la Wanatheolojia wanatafakari kwa makini jambo hili ili kulitolea ufafanuzi kipindi hiki ambacho uandishi rasmi wa historia halisi ya kanisa iliyoidhinishwa na halmashauri kuu ya TAG, unaendelea.

uongozi wa TAG, unawaomba wachungaji na washirika wasiyumbishwe na maudhuhi ya kitabu hicho.

kwa kuwa ni historia ya TAG, kanisa lenyewe lilipaswa kushirikishwa, lakini jambo hilo halikufanyika, hivyo kitabu hicho si halali.

limetolewa na
KATIBU MKUU WA
TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD

No comments:

Post a Comment