OTHER WEBSITE LISTS


Tuesday, July 26, 2011

Sitasau nilivyowatoa watoto wangu kafara -

Karibu tena kwenye safu yetu hii ya shuhuda za yale yaliyotokea katika ulimwengu wa wasioamini (waabudu shetani) katika mkasa huu ndugu Renatus Mungai anashuhudia kwa machozi akiwa mafichoni yale aliyokumbana nayo katika maisha yake wakati akimtumikia shetani. Wiki iliyopita tuliona jinsi alivyokuwa akimhadaa mkewe ili kupata nafasi ya kumpeleka mtoto wake wa kwanza kwenye hekalu huko Nairobi ili kutimiza matakwa ya master (mkuu wa hekalu la Freemasons) mkasa wa ndugu huyu pamoja na mengine iliripotiwa kwenye magazeti hata ikamsukuma aliyekuwa Rais wa Kenya Daniel Moi, kuunda tume ya kufuatilia ibada ya mashetani Kenya ambayo ilifika hadi Tanzania na kuhoji watu kadhaa akiwepo mfanyabiashara mashuhuri . wiki hii anaendelea na kipengere hicho. Tafadhali ungana naye.


Kabla ya kuendela na ushuhuda wa Renatus, hebu nikuletee jumbe kadhaa za wasomaji wetu wanaotoa maoni yao ambzo zimetumwa kwa mhariri kupitia, Mail, SMS na simu za mkononi.
Miongoni mwa wale waliotuma jumbne hizo ni Dada Helen Mkama, kutoka musema ambaye alisema: “Tafadhali mhariri najua itakuwa shida kidogo kuonana na Ndugu Renatus, lakini naomba mfikishie ujumbe huu, tena nadhani ni vyema ukauchapisha kwenye gazeti kwa kuwa sio yeye pekee wako wengi walioingizwa au kujiingiza kwenye ibada za shetani kwa
tama ya fedha lakini sasa wako hatiani, wanalia machozi na kusaga meno.
Ndugu Renatus kwanza pole kwa yaliyokukuta.., nakupa ushauri ujitie moyo usirudi nyuma kamwe hatakama watafanikiwa kukutia mikononi usilikane jina la Yesu tena kwa kuwa kufanya hivyo utakuwa umejitumbukiza kwenye dhambi ya kukufuru Roho mtakatifu isiyosamehewa. Najua unapitia kipindi kigumu kwa kuwa umekula vya ibilisi na sasa anataka ulipe gharama. Kuwa tayari hata
kufa pamoja na Kristo kuliko kuishi na shetani ukitarajia kutupwa pamoja naye katika ziwa la moto.
Ujumbe kwa wasioamini kuwepo kwa ibada za mashetani, nawashauri wafungue kurasa za mtandao waingine kwenye ule mashuri wa Google, kasha waandike neno “Satanic worshipers” au Freemason and “Satanic worshipers”. Natumaini hawatashangaa watakapoiona Bibklia ya shetani na
amri zake kumi kama za Mungu na jinsi watu wanavyofanya ibada za kishetani na mipango ya kungusha watakatifu.
Mimi nilikuwa miongoni mwa wale wanaokataa kuhusu ibada za kishetani, lakini mume wangu ambaye ni mwanafunzi wa shahada ya pili katika
chuo kimoja cha Marekani alinitumia anuani hizo na kunieleza kuwa yeye binafsi bila ya kujua alishaingia kwenye hekalu la Freemason mjini Washington na kushuhudia mambo ya kustaajabisha. Mambo haya ni kweli na ni hatari ni heri kusikia tukajua na kuonya watioto wetu tukiwaelekeza jinsi ya kukwepa hatari hii. Bibilia inatuambia kuwa shetani ni anazunguka sunguka kama samba angurumaye akitafuata mtu ammeze.”

Baada ya ujumbe huu hebu sasa ungana na Renatus katika ushuhuda wake:
Baada ya kumpa ile soda niklikuwa makini kuhakikisha kuwa mlango wa gari umefungwa vizuri ili usije ukafunguka akaanguka wakati gari likiwa kwenye mwendo nilikuiwa nikiendesha gari huku nikimtizama kwa makini kuona kile kitakachotokea.
Nilikuwa na uhamkika kuwa atalewa mapema kwa kuwa si mtu wa vileo, na wala hajawahi kunywa pombe tangu nilipomuoa . baada ya muda niliona akiefgemea kwenye kiti nikajua mambo yameiva….nuilisimamisha gari na kulaza kiti chake ili alale salama wakati nikiendelea kutimiza wajibu wangu kwa wakuu wa hekalu.
Nilipohakikisha kuwa amelala sawa sawa niliendesha gari kwa kasi hadi hekaluni ambapo nilipaki na kumchukua mtoto nikatoka naye na kumwacha kwenye gari . nilienda moja kwa moja hadi hekaluni ambapo mtoto alipokelewa na wahudumu wakampeleka kwa master ambaye alimpokea na kumtazama kwa makini kasha akasema:
“Hekalu limejipatia mkadhao ya utiifu wetu…..leo hii mtoto huyo tunamuweka wakfu kuwa mtumishi wa madhabahuni na atatumikia mamlaka kuu zaidi ya ulimwengu huu akiwa mjenzi mwaminifu kwa ulimwengu huru …..hatafungwa na taratibu za watu waliojitungia iliwatawale wengine.”
Kisha alichovya kidole kwenye mvinyo akadondosha tone moja la mvinyo uliotiririka kutoka kidoleni kwenye paji la uso la mtssoto na kumuita: “ Andy……..umekabidhiwa kuwa motto wa madhabahuni kama ilivyo kwa baba yako, utalindwa na kutunzwa kwa gharama ya damu.”
Kisha alinigeukia na kuniita: “Renatus motto huyu tangu leo si wako wala mtu mwingine ni
mali ya madhabahu na itahusika na gharama zake zote kwa kuwa ni mtenda kazi mtarajiwa ……mlee katika kanuni zote zinazostahili na namba yake ni 0066. Hii utaitumjia kuchukua mahitaji yake yote.”
Suala la namba hiyo halikuwa gumu kwangu mimi mwenyewe nakumbuka nilipopelekwa hekaluni na babu nilipewa namba 0026, na ni namba hiyo ilikuwa ikinitambulisha popote nilipokutana na wenzangu na hata malipo yangu kwa ajili ya masomo harusi na mambo mengine yalitoka kwa namba hiyo.
Baada ya kukamilisha zoezi
hilo niliitwa na master na kuambiwa kuwa ninatakiwa kuwa makini sana kwa kuwa kama nitavujisha siri zabngu kwa mke wangu ambaye haamini ulimwengu huru hakika atakufa kwa kuwa moyo wake ni mwepesi hauwezi kuhimili mambo ya hekaluni.
Nilimhakikishia master kuwa hatajua na nitailinda siri hiyo kwa gharama ya damu. Labada ni fafanue kidogo maana ya kiapo cha gharama ya damu. Unapokuwa umeapa kwa gharama ya damu inamaanisha kuwa damu ya mtu kama fidia itamwagika ili kufuata dhambi husika. Mara nyingi mkosaji hafi ila anauliwa mtu wake wa karibu kama adhabu itakayokuwa onyo kwake na kwa wengine ambao ni wanachama .
Baada ya mazungumzo hayo nilipewa vocha yenye namba yangu nay a m,toto ambayo iliandikwa hivi: 0026+0066, akaniwsambia kuwa niende kwenye benki ya ……..(jina la benki husika tunaklihifazi kwa sababu za kisheria) nitakuwa nikipokea malipo kwa ajili ya motto kila mwezi. Banki hii ambayo imeenea funia kote ni mali ya kundi la Freemason na ndipo mahakli malipo yao yanapopitia.
Nilipomaliza kuagana na master nilirudi kwenye gari na kukuta mkewangu ndio kwanza usingine unamzidia …….nikaendesha gari mpaka nyumbani nikamshusha na kumuingine chumbani nikamuweka kitandani, nikimuangalia.
Nilipoangalia saa yangu ilikuwa majira ya saa tano na nusu hivi na mtoto alianza kulia nikajua ni njaa nikmkorogea maziwa na kumpa akala kidogo lakini sikuwa najua ni kiasi gani hasa anapaswa kunywa mtoto wa umrio ule kwa hiyo nikamuacha nikiwa sina uhakika kama ameshiba au laa. Ilipofika saa saba nilimpa tena akala kidogo na kuendelea kulala. Wakato wote akili yangu ilikuwa inazunguka nikifikiri ni kwanini haamki na muda mrefu umepita.
Ilipofika saa tiza na nusu motto alinza kulia nikimpa maziwa aligoma kunywa kabisa huku akilia kama anayetaka kukata roho, nuikamuweka mgongoni kwa nikimfunga kwa shuka kwani nilihofia kanga isingezunguka vizuri na kumshikilia na mimi sikujua m,ahali vitenge viluipo na wala muda wa kutafuata sikuwa nao.
Nilihangaika kumbembeleza lakini wapi, alikuwa akizidi kulia, ni hapo nilipogundua umuhimu wa mama kwenye familia kwa undani zaidi kuliko ambavyo nilikuwa nikidhani. Nilimpigia yule rafiki yangu master mind aliyeniambia jinsi ya kumlewasha mke wangu…..nilipoongea naye alikuwa anacheka na kuniambia : “Reni nilidhani wewe mwanaume kumbe hamna lolote……unaongea kama mtoto? Chukua maji ya uvugu vugu mnyweshe mtoto atatulia na kulala, akishalala chukua ndimu au limau mkamulie mkeo mdomoni kasha muache kwea dakika kadhaa ataamka.”
Nilitii maelekezo hayo na kuchukua maji ya vugu vugu kwenye chupa ambayo mama yake alikuwa amechemsha ya kumuogeshea nikampe akanywa kama vijiko vitano hivi akalala ……nikapata nguvu nikaenda kwenye friji na kuchukua limao nikamkamulia mkewangu mdomoni kama nanywesha mgopnjwa huku roho ikiniuma. Baada ya zoezi hilo nilitulia dakika tano hivi nikachikua maji baridi na kumnawisha uso. Ghafla nikaona anafungua macho na kufunga mdomo ambao aliuacha wazi
mda mrfu sana. Nilimuacha mpaka akachangamka , nikamwambia pole kwa usingize mzito.
Alinitazama kwa muda na ghafla akaniuliza mtoto wangu yuko wapi? ……kwani ni saa ngapi ?

Itaendelea

No comments:

Post a Comment